1. Ugumu katika kufunguka.
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana tena sana
kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni
wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndoa mkaitwa
sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia
mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na
kummaliza.
2. Ugumu katika kusamehe.
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya
ya wewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu,
hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote.
Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu
sana kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha
uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.
3. Msongo wa mawazo.
Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo
“stress” ingawa kwa nje wanajitahidi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari
wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda
au ya kushuka, stroke, kusimama kwamoyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo
ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani. Kuwa open, roho
safi and less aggressive.
4. Ugumu katika kujali afya.
Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende
hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa
au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe
mwongo.Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.
5. Tabia hatarishi.
Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza
kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka
karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa
wako mkutanoni mkoani.
No comments:
Post a Comment