Dunia hii Kuna kupenda na kupendwa, kupata na kupatikanka,
kuwekeza na kuwekezwa na kuchumbia na kuchumbiwa.
Kwa hali halisi inayoaminiwa binadamu walio wengi ni vigumu
sana kumsahau na kuacha mapenzi au mpenzi wa awali.Hii Inasemekana ipo sana kwa
wanawake, anaweza kuwa ana mtu wake vizuri lakini anapokuja mpenzi wa zamani
ambaye alipenda basi lazima atafanya njia yoyote ile wakutane. Ni vigumu kuacha
mapenzi ya awali kwa walio wengi.
Hii imemtokea rafiki yangu ambaye alimfuatilia sana dada
mmoja kwa muda sana na mwishowe akampata, wamekaa na kupendana sana na wamedumu
mpaka leo, ni mfano wa kuigwa na kilichobaki tunasubiri Ndoa.Kama ilivyo ada
kwa mwanaume ukipata mwanamke mzuri basi matunzo hayatakuwa mbali, jamaa kamtafutia
na kazi huyo mpenz wake baada ya kumaliza chuo.Kama ni la kupostiwa insta,
facebook, kumweka dp hadi tumezoea.
Kinachonisikitisha leo, Kuna mdada mmoja ambaye pia ni rafiki
yangu wa mda mrefu, ni mtu ambaye ananisaidia mengi kwenye ushauri, Akaniambia
mdogo wangu(yaani mdogo wake) yupo hapa na mchumba yake, kwa vile namjua vizur
kwa sababu tuliwahi kukaa wote kijj kimoja Huko mkoani. Basi tunasalimiana pale
na nilipomuuliza vipi nimesikia uko na mchumba wako hapo, Akanijibu ndio niko
na mchumba wangu(akamtaja jina), nkahamaki kisha nkamuliza huyo mchumba ni wa
wapi, akasema yule wa kule nyumbani karibu na sokoni nyumba ya juu,
Nikamuuliza mmeanza lini, akasema huyu mbona mpenzi wangu
toka shule ya msingi pale(akataja shule), nikamuuliza mara nyingi lakini ukweli
ukabaki pale pale kuwa huyu ndo yule ambaye jamaa kamweka profile picture
sehemu nyingi za mitandaoni. Mimi na huyo mwanamke tunafahamiana vizuri maana
jamaa alipokuwa anatongoza miaka hiyo huyo mwanamke tulikuwa tunasoma shule
moja. Bahati nzuri wakat maongezi yanaendelea yeye alikuwa na wifi(Rafiki
yangu) yake wako ndani wanaandaa chakula
Hapo nilipoamini pamoja na kumfanyia huyu mdada kila kitu,
ila first love yake bado haijafa.
No comments:
Post a Comment