Ukiona dalili hizi ujue ashadata kwako

1. Atakutega kupata attention yako.Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda au lah! Mf wa mambo hayo ni kujifanya anaumwa na kuangalia respond yako kwake ni kiasi gani unamjalina kiasi gani utahangaika kwa ajili yake.
2. Haoni aibu kugusa sehemu yako yamwili. Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomosa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia zakushikana kwenu kutamrahisishia kazi yakuwa na wewe.
3. Kucheka kwa nguvu hata kwa kitukisicho chekesha endapo wewe umezungumza. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli.
4. Wivu hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachat nao na ukiwaita majina ya kimahaba hapendi.
5. Anakumbuka siku zako muhimu.Hukumbuka kama vile siku yako yakuzaliwa hatoweza kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifaulu mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza.
6. Eye contact anapenda kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utaelewa ni kiaisi gani anakupenda kupitia vile ambavyo anakuangalia.Ila wengine huona aibu kuwatazamawavulana wanaowapenda si wote wanaujasiri wa kuwatazama wapenzi wao.
7. Hupenda kukaa mudamwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bilakuchoka. Anaweza akaacha kila kituanachokifanya ili ajumuike na wewe.
8. Yupo tayari kuangamiza kama msichana anakupenda yupo tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtumwingine. Utaona vipi huyo msichana alivyo kwako na wa wengine.Yaani yupo tayari yeye akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwambia hana alichoombwa, lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine.
9. Anachukulia matatizo yako kama ni yake. Unapomueleza kuwa ana tatizo anajali tatizo lako kama vile ni lake na hujisikia vibaya sana na kuhuzunika na atafanya lolote ili aweze kukusaidia utoke katika hilo tatizo.

10. Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakuambia anakupenda. Kwa kuwa anakupenda endapo ikatokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose.

No comments:

Post a Comment