Nikisema mtu toxic namaanisha wale watu ambao wanakuumiza
akili, moyo, confidence yako na hata mawazo yako. Hizi ni dalili 5 tu ambazo zitakusaidia
kujua kuwa huyo mtu ambaye upo naye katika mahusiano ni toxic ama la.
1.Katika malumbano kati yenu yeye huwa anataka kukuumiza
wewe na sio kusuluhisha tatizo kati yenu.
Jamani ndugu zangu, mnatakiwa kujua kuwa ili mahusiano yenu
kuwa mazuri, kuwa perfect, wewe na mwenza wako mnatakiwa mtafute njia ya
kusuluhisha matatizo kati yenu. Lakini kama kila ukigombana na mwenza wako yeye
always anatafuta tu njia ya kukuumiza wewe basi that person is TOXIC.
Haimaanishi kuwa hamtakiwi kugombana, kila mahusiano kuna matatizo.
2.Wanafanya kila kitu kama ni mashambulizi.
Mfano ukienda kwa mwenza wako na ukataka kuongea naye kuhusu
kitu ambacho hukupendezwa nacho, labda kitu alichofanya this week au
alichosema. Unaweza ukamuendea kwa upendo wote lakini yeye akachukulia vibaya.
Ili kujua hili,
fikiria kwa sasa katika mahusiano yenu, Je unauhuru wa kumuendea mwenza wako
kuhusu jambo lolote? Huna uwoga kwamba nikimuambia kitu fulani ataishia
kukasirika tu, kama huwezi basi ujue kuwa haupo kwenye uhusiano salama.
3.Wanakufanya wewe ndio sababu ya kila tatizo katika
mahusiano yenu.
Hapa inakuwa kila tatizo, kila kitu kibaya kitakachotokea
ndani ya mahusiano yenu ni kosa lako, wewe ndio utakuwa unalaumiwa kwa kila
kitu. Utaambiwa kuwa wewe ndio tatizo na wewe ndio huelewi. Badala ya kukubali
kuwa yeye ndio amefanya kosa ni lazima tu atatafuta njia ya kugeuza mambo na
kukufanya wewe ndio uonekane ndio mwenye kosa.
Toxic people yani wanajua kudanganya na kuendesha watu.
Wanaweza kukufanya kuwa wewe ndio mwenye tatizo hata kama yeye ndio mwenye
kosa. Ukimuacha mtu kama huyo kuendelea kukuendesha au ukiendelea kuwa katika
mahusiano na mtu kama huyo ni lazima ataharibu ujasiri wako, no matter how
strong and confident you are.
4.Atakuonesha upendo mkubwa sana pindi ukiwa chini.
Tatizo kubwa la toxic people ni kuwa baada ya kukuumiza,
kukusingizia vitu, kukufanya ujisikie huna maana, ( ndipo watakufanya uamini
kuwa yeye tu ndio anakupenda, kuwa hakuna mtu mwingine zaidi yake yeye
atayekupenda, na ukiamini hiki ndio kinampa nguvu ya kukufanyia chochote
anachotaka ). So baada ya kukuumiza na wewe ndio upo at your lowest point, hapo
ndio atakuonesha upendo kubwa zaidi ya siku zote, akishagundua kuwa umeumia
ndio na yeye hujishusha.
Hii ni kwasababu katika kipindi ambacho wewe unaujsari na
huumii, yeye anajiona kama hana nguvu juu yako, na hivyo anataka yeye ndio awe mwenye nguvu.
5.Anakuwa hana Furaha na mafanikio yako.
Atakushusha hata kama unafanya vizuri katika maisha yako, ni
lazima tu atatafuta njia ya kukufanya uone kuwa mafanikio yako sio ya muhimu,
like it is not a big deal. Hata kama umefanikiwa kupata kitu ulichokuwa
unakifanyia kazi kwa muda mrefu, kamwe hatosherekea na wewe, atabadilisha
topic, na kuanza kuelezea kitu kingine au atatafuta tatizo lolote tu.
Hii ni kwasababu toxic people wanapenda wewe uwe
chini, usimpite kwenye chochote, iwe mshahara mnayopokea, mafanikio mnayopata,
furaha yaani kwa kila kitu yeye ndio anataka kuwa juu yako. Yeye tu ndio
anataka awe mtu anayekupa furaha ndio maana atakuweka chini kwa kila jambo zuri
litakalokutokea ili ukisha-break sasa yeye ndio apate nafasi ya kuja
kukunyanyua tena.
No comments:
Post a Comment