Hii ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na
hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya
nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika,
wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo.
Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia
ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.
(2) Wanaume wanaojihisi bado hawajaoa (Bachelor Husband);
Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa
chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na
marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui, mke anaweza kustukizia tu
mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza
kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki
kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.
(3) Wanaume wenye gubu (Acidic Husband);
Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya msingi,
mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini
hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni
shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke.
(4) Mume wa kila mtu (General Husband);
Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke,
wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke
anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki
wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia
wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.
(5) Wanaume wanaojifanya wagumu (Dry Husband);
Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba
na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna
kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali
wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma
sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi
yoyote kuwafurahisha wekea zao.
(6) Wanaume wanaopenda kutumia wake zao (Panadol Husband);
Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na
wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke,
wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata
kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai
kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama
wanawake, hawajali tena.
(7) Wanaume ambao hawataki kukua (Baby Husband);
Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao
wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu
Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize
ndugu kwanza ndiyo kipitishwe na mke akifanya kosaakidogo kazi nikulinganisha
mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na
mambo kama hayo. Kwa kifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa
Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa.
(8) Mume Mtalii (Visiting Husband);
Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia
familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto
wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki
hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja
ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya
kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto.
(9) Wanaume wanaofuatilia kila kitu (Stalking Husband);
Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu,
huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu
atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu
na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa
jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi
wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke.
(10) Mwanaume mbahili (Miserly Husband);
Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa
mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia
mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha anataka ajue iliisha ishaje na kila mara
huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu
kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa
na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.
Hiyo ni baadhi tu ya aina ya wanaume ambao wanawake wengi
wasingependa kuwa nao. Kama mwanaume upo hivyo jua mke wako hafurahii na
anavumilia tu. Ndoa ni furaha amua kubadilika na usimfanye mke wako kuishi na
wewe kwa kujilazimisha. Kama ni mume jiulize uko namba ngapi hapo na kama ni
mke mezea namba ya mumeo.
No comments:
Post a Comment