.Mapenzi yanaumiza #True story


Ni kutoka kwa rafiki yangu, ambaye mpaka sasa ni kama karukwa na akili, huongea mwenyewe hata kucheka ovyo mpaka ana huzunisha.
Ni  kwamba huyu rafiki yangu mkubwa, alikutana na binti mmoja huko Iringa alipokua field, ambaye alitokea kumpenda sana, kutokana na life style yao pale kijijini alipokuwa anafanya field kwa moyo mmoja aliamua kumsaidia na kwa kipindi hicho jamaa ndio kamaliza chuo.
Wazungu wanaita love at a first site ndicho kilicho mtokea rafiki yangu alikufa na kuoza kwa huyo binti.
Siku zilipita na field ikaisha,binti akarudi nae mjini akamfanyia mpango akaanza kusoma kozi ya flight attendants chuo kimoja kipo posta pembeni ya sanamu la askari. Binti alisoma kwa udhamini wa jamaa. Binti alimaliza certificate kwa bahati nzuri akaendelea diploma bado jamaa alikuwa anadhamini huku wakipeana ahadi za kuwa wataoana kwani aliona ni binti wakuoa na mwenye maadili.
Kumbe sivyo alivyofikiria, binti baada ya kumaliza diploma jamaa akafanya mpango akapata ajira kwenye shirika moja la kigeni kama mhudumu wa ndege, ndipo balaaa likaanza binti alianza  kuwa na kiburi huku akisahau alipotoka.
Wiki iliyopita binti kamwambia jamaa hampendi na asante kwa kumsomesha ila amepata anayempenda zaidi. Na kwa taarifa aliyopata jamaa ni kwama binti kapewa ahadi ya kusomeshwa chuo kinachomilikiwa na ndege za Emirates so ndio kapata kiburi, na ni wiki sasa binti kakata mawasiliano na kamblock jamaa.
Ninavyoandika hapa jamaa kama kawehuka haamini kilicho mtokea, jamaa anaongea hovyo hovyo ila yote ni sababu ya binti aliyemtoa kijijini na kumsomesha akiamini atakuwa mke wake ila leo kamgeuka.

Wanawake kuweni na huruma jamani jueni mnaonekana.

No comments:

Post a Comment